Wednesday 20 February 2013

Mapishi ya Pizza


Vipimo:
  • Unga.......................... ..4 Vikombe
  • Maziwa ya unga.............2 vijiko vya supu
  • Mafuta ya zaituni...........½ kikombe
  • Hamira........................ .1 kijiko cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Sukari........................ ..1 kijiko cha chai
  • Maji vugu vugu..............2 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Unga
  • Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
  • Ufunike na uache uumuke.


Sosi Ya Pizza
1. Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo .. 1
2. Thomu iliyokatwa ndogo ndogo ....... 3 chembe 
3. Sosi ya HP .............................. .... 3 vijiko vya supu
4. Sosi ya tomato ............................. 3 vijiko vya supu
5. Pilipili manga .............................. ... 1 kijiko cha chai
6. Oregano .............................. ........ ½ kijiko cha chai
7. Parsley (ukipenda) ......................... ½ ukipenda

1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
2. Epua kwenye moto.

Upendavyo Katika Hivi Au Vyovyote Vinginevyo
1. Tuna 
2. Nyama ya kusaga iliyopikwa 
3. Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande 
4. Sauage zilizokatwa 
5. Salami 
6. Vipande vya nanasi

Vitu Vya Kujaza Juu Ya Pizza
  • Nyanya zilizokatwa vipande vipande
  • Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
  • Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
  • Cheese ya Mazorella


Jinsi Ya Kutayarisha
1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size kama kwenye picha.
2. Paka sosi juu ya unga
3. Tia kiteo upendacho
4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
5. Mwagia cheese
6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive pizza.

No comments:

Post a Comment